1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la UN lataka kusitishwa kwa mzingiro El-Fasher

14 Juni 2024

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linalotaka kusitishwa kwa mzingiro wa kijeshi kwenye mji wa Sudan wa El-Fasher pamoja na kumalizwa kwa machafuko nchini humo.

https://p.dw.com/p/4h2P5
Sudan
Vita vya Sudan vimeendelea kuwahangaisha wakaazi na kusababisha janga kubwa la kibinaadamu Picha: AFP

Sudan imeghubikwa na vita kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Wanachama 14 kati ya 15 wa Baraza la Usalama walipiga kura kuunga mkono azimio hilo lililoandaliwa na Uingereza. Urusi ilijizuia kulipigia kura azimio hilo.

Azimio la kupinga mzingiro wa mji wa Al-Fashir kupigiwa kura

Azimio hilo linatoa wito kwa pande mbili zinazozozana, ambalo ni  jeshi la Sudan na kundi la wanamgambo la RSF kusitisha mara moja mapigano.

Pande hizo hasimu zimekuwa zikipambana kuwania udhibiti wa El-Fasher ambao ni mji mkuu wa mkoa wa Darfur Kaskazini.