SiasaUkraine
Baraza la Usalama la UN lakutana kuijadili Ukraine
30 Desemba 2023Matangazo
Mashambulizi hayo ya Urusi yamewauwa raia 31 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 160, kulingana na maafisa, huku Poland ikisema kombora la Urusi lilirukia katika anga yake kabla ya kurejea Ukraine.
Soma pia:Watu 24 wauawa Ukraine katika wimbi jipya la mashambulizi
Baada ya kuanza kwa mkutano huo, wanachama wa baraza hilo Marekani, Ufaransa na Ungereza zililaani mashambulizi dhidi ya Ukraine. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, pia alilaani mashambulizi hayo kwa mujibu wa msemaji wake Stephane Dujarric.