MigogoroSudan
Baraza la Usalama la UM kujadili vita vya Sudan
18 Novemba 2024Matangazo
Hayo yanajiri wakati ambapo vita kati ya majenerali wawili wanaohasimiana havionyeshi dalili zozote za kufikia kikomo.
Muswada huo ulioandaliwa na Uingereza na Sierra Leone, unatoa wito kwa wahusika "kusitisha uhasama mara moja na kushiriki kwa nia njema katika mazungumzo ya amani ili hatimaye kufikiwa mpango wa usitishwaji mapigano.
Soma pia: Watafiti wasema huenda vifo Sudan ni vingi zaidi ya vinavyoripotiwa
Sudan imeharibiwa na vita tangu Aprili mwaka 2023 kufuatia mapigano kati ya jeshi la la Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye alichukua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2021, na Kikosi cha RSF kinachoongozwa na naibu wake wa zamani, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.