1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Seneti laanza kujadili hoja ya kuondolewa Gachagua

16 Oktoba 2024

Baraza la Seneti nchini Kenya limeanza Jumatano (16.10.2024) kujadili muswada uliopitishwa na Bunge kuhusu kuondolewa madarakani kwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua.

https://p.dw.com/p/4lrSK
Baraza la Seneti nchini Kenya laanza kujadili hoja ya kuondolewa madarakani Gachagua
Baraza la Seneti nchini Kenya laanza kujadili hoja ya kuondolewa madarakani GachaguaPicha: Andrew Kasuku/AP/picture alliance

Mahakama Kuu ya Kenya ilitupilia mbali hapo jana ombi la mwanasiasa huyo aliyetaka hoja hiyo kuzuiwa na isiendelee kujadiliwa kwenye Baraza la Seneti, akidai kuwa hoja ya kumtimua ilitokana na madai ya uwongo yaliyochochewa kisiasa.

Lakini Mahakama hiyo imesisitiza hivi leo kuwa mchakato huo ni wa kikatiba na haitouingilia kabisa.

Wiki iliyopita, wabunge walipiga kura ya kumuondoa madarakani Gachagua, kwa madai ya kuchochea chuki za kikabila, ubadhirifu, na kuidhoofisha serikali, hatua iliyofungua njia kwa Baraza la Seneti kuanza kulijadili suala hilo.