1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la mawarizi la Iraq laidhinisha kuongezwa kwa muda wa Jeshi la Marekani.

Eric Kalume Ponda17 Novemba 2008

Baraza la Mawaziri nchini Iraq hatimaye limeidhinisha mpango uliofanyiwa marekebisho wa kuendelea kuhudumu kwa vikosi vya usalama vya Marekani nchini humo hadi mwaka 2011.

https://p.dw.com/p/Fwhy
Wanajeshi wa Marekani wakishika doria nchini Iraq. Huenda wakasalia nchini humo hadi 2011 iwapo mpango mpya utaidhinishwa na bunge.Picha: AP


► Baraza la Mawaziri nchini Iraq hatimaye limeidhinisha mpango uliofanyiwa marekebisho wa kuendelea kuhudumu kwa vikosi vya usalama vya Marekani nchini humo hadi mwaka 2011.




Hata hivyo bado mpango huo nunasubiri kuidhinishwa na bunge, ingawa unakabiliwa na upinzani mkali na huenda haitakuwa rahisi kuwashawishi raia wa nchi


Kuidhinishwa kwa mpango huo na baraza la mawaziri mnamo siku ya Jumapili iliyopita, huenda kumefungua ukurasa mpya wa mvutano miongoni mwa wabunge, wakati mpango huo utakapoanza kujadiliwa wiki hii.


Kulingana na muda wa mwisho ulioafikiwa na umoja wa mataifa , jeshi la muungano nchini Iraq linapasa kuanza kuondoka mwishoni mwa mwaka huu.


Hata serikali ya waziri mkuu wa nchi hiyo Nuri Al Maliki, kwa kuidhinisha mpango, jeshi la Marekani linapasa kuendelea kuhudumu nchini humo hadi mwaka wa 2011, hatua inayopingwa vikali na wabunge wafuasi wa kiongozi wa dhehabu la Washia, Moqtada Al- Sadr.


Wafuasi wa kiongozi huyo ambao ni idadi ya wabunge 30 katika bunge hilo la Iraq, wanasema kuwa watawasilisha mswada bungeni kutaka kufanyiwa marekebisho kwa kifungu cha sheria ili mpango huo uweze kuidhinishwa na theluthi moja ya wabunge na wala sio wingi wa wabunge bungeni.


Kadhalika wabunge wafuasi wa kiongozi huyo Moqtada al Sadr, ambao wamekuwa wapinzani wakubwa wa kuendelea kuwepo kwa majeshi ya kigeni katika ardhi ya Iraq baada ya kumalizika kwa muda huo uliowekwa na Umoja wa mataifa,wanasema wataandamana kupinga kuweko zaidi kwa majeshi ya kigeni nchini humo.

Maandamano hayo yanayokusudiwa kuwahamasisha, na pia kutafuta kuungwa mkono kwa wabunge wa Shia miongoni mwa raia wa Iraq, huenda yakawa na athari kubwa katika siasa za nchi hiyo, huku inapojiandaa kwa uchaguzi wa majimbo hapo januari 31.

Wafuasi hao wanasema kuwa watatumia ushawishi wao katika bunge hilo lenye wabunge 275 kupinga mpango huo unaotarajiwa kujadiliwa kwa muda wa wiki nzima, kabla ya kupigiwa kura Novemba 24.

Endapo mpango huo utaidhinishwa na bunge, utahitaji kuratibiwa na rais wa nchi hiyo kabla ya Waziri mkuu Nur al Malik na Rais George W Bush kuutia saini.

Hatua hii imetokea huku rais mteule wa Marekani Barrak Obama anapoendelea kuisuka serikali yake kabla ya kuapishwa madarakani hapo jamnuari 20.


Iwapo mpango huo utaidhinishwa na bunge la Iraq huenda hii itakuwa kinyume na msimamo wa Rais huyo mteule Barrak Obama ambaye amekuwa akisisitiza kuondolewa kwa majeshi ya Marekani nchini Iraq.


Tayari Rais huyo mteule alikuwa na mpango wa kuondolewa kwa vikosi vya Marekani nchini Iraq kwa awamu ya vikosi viwili kwa mwezi.