Baraza la kitaifa latangazwa nchini Guinea.
24 Desemba 2008CONAKRY.
Wanajeshi waliotwaa serikali nchini Guinea wametangaza baraza la kitaifa lenye wajumbe 32.
Baraza hilo la mpito ndilo litakaloongoza nchi. Wanajeshi hao wameiangusha serikali muda mfupi baada ya kifo cha rais Lansana Conte.
Mkuu wa baraza hilo atakuwa kiongozi wa wanajeshi waliotwaa serikali, kapteni Mussa Dadis Camara.Raia sita pia wameteuliwa kuwamo katika baraza hilo.
Hatahivyo spika wa bunge Aboubacar Sompare amesema anaamini kuwa wanajeshi waliojaribu kutwaa serikali ni watu wachache na kwamba hawaungwi mkono jeshini.
Wakati huo huo ,Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika linakutanakujadili hali ya nchini Guinea kufuatia hatua ya kundi la wanajeshi kujaribu kuianhusha serikali.