Baraza la katiba Chad lakataa kufuta matokeo ya uchaguzi
16 Mei 2024Matangazo
Baraza la Katiba nchini Chad limeyatupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na wagombea wawili walioshindwa kwenye uchaguzi wa rais, ya kutaka matokeo ya uchaguzi huo yabatilishwe.
Baraza hilo limesema wagombea hao wameshindwa kutowa ushahidi kuunga mkono madai yao kwamba ulifanyika udanganyifu.
Tume ya uchaguzi wiki iliyopita ilimtangaza mshindi rais wa mpito Mahamat Idriss Deby wa uchaguzi huo wa rais, kwa kupata asilimia 61.3 huku Masra akichukua nafasi ya pili kwa kujipatia asilimia 18.53 ya kura, kulingana na matokeo ya awali.