Baraza la Haki za Binadamu lakutana Geneva
1 Juni 2012Tuhuma za awali zikidai mauaji hayo yamefanywa na wanajeshi wanaomuunga mkono Rais Bashar al-Assad. Serikali yake inakidai mauaji hayo yalifanywa na jeshi la ukombozi wa Syria linalotaka kumng'oa madarakani Kiongozi huyo.
Mataifa 47 yanakusanyika katika jiji la Geneva kikiwa ni kikao cha nne kwa mwaka huu juu ya Syria tu, taifa lililo katika machafuko kwa mwaka mmoja sasa huku vifo vya watu wasio na hatia vikiendelea kutokea kila uchao na kupoteza uhai wa maelfu.
Tukio la hivi karibuni ni mauaji ya watu 108 wakiwemo wanawake na watoto.
Nakala ya Azimio hilo zilisambazwa jana zimeonyesha kuwa Baraza la Usalama la umoja wa mataifa kwanza linalaani mauaji hayo ambayo yalifanyika katika makaazi ya raia.
Maamuzi ya baraza hilo yanatazamwa kuwa yanaweza kuja na muafaka wa utatuzi wa hali ya Syria japokuwa kuna dalili za China, Cuba, Urusi kuweza kupinga maamuzi yatayakayoamuliwa. Hali ya kupin´gana inatarajiwa na maafisa wa kidiplomasia kutoka nchi za kiarabu na nchi kadhaa za magharibi.
Pande zote zatuhumiwa
Akizungumzia hali halisi ya Syria, Afisa wa Baraza hilo, Navi Pillay amesema kuwa mauaji yaliyotekea katika mji El-Houleh yalifanyika katika makaazi ya watu yanasadikiwa kufanywa na kikosi cha Assad kijulikanacho kama Shabbiha.
Lakini afisa huyo amewatuhumu wapiganaji wanaoupinga utawala wa Assad wanafanya mauaji ili kuishawishi jumuiya za kimataifa itumia nguvu za kijeshi dhidi ya utawala wa Assad.
Mashaka kwa wanadiplomasia
Wanadipolmasia wa Ulaya pia wanaona kuwa ili kufanikisha utatuzi wa mgogoro huo ni vyema Urusi kuhusishwa kwa karibu na kuunga mkono maamuzi hayo ilikuweza kufanikisha utekelezaji wake kwani uamuzi wa kura ya turufu yaani Veto ya Urusi unaweza kuwa na changamoto kubwa katika kupata azimio muafaka kwa taifa la Syria.
Kwa sasa Ujerumani na Ufaransa zinaonekana kutoa msukumo mkubwa ilikuweza kumshawishi Rais Vladimir Putin lakini hakuna dalili zozote za Urusi kuweza kuja na maamuzi ya kumshinikiza koo Rais Assad na utawala wake .
Changamoto kubwa ni kwamba kwa hakika Ujerumani, Ufaransa na Urusi kwa pamoja ni wajumbe wenye kura ya maaamuzi katika Baraza hilo la haki za binaadamu huko China nayo ikielemea upande wa Urusi.
Mwandishi:Adeladius MakwegaAFP/RTRE/APE/AFPE
Mhariri: Moahammed Abdul-Rahman