1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Barani la Ulaya mwenyeji wa fainali za kombe la dunia 2018

Sekione Kitojo1 Desemba 2010

Kwa mara ya kwanza katika historia yake shirikisho la kandanda duniani , FIFA , litachagua wenyeji wawili wa mashindano tofauti ya fainali za kombe la dunia kwa wakati mmoja.

https://p.dw.com/p/QNXw
Rais wa shirikisho la kandanda FIFA Joseph Sepp Blatter.Picha: picture alliance/Photoshot

Kwa  mara  ya  kwanza   katika  historia  yake  shirikisho  la  kandanda duniani,  FIFA,  litafanya  uchaguzi  wa  nchi  mbili  zitakazokuwa  wenyeji wa  mashindano  ya  shirikisho hilo. Kamati  tendaji  itachagua  leo  Desemba 2  mjini  Zurich  nchi  wenyeji  wa  mashindano  ya  soka  kwa  ajili  ya fainali  za  kombe  la  dunia  kwa  mwaka  2018  pamoja  na  fainali  za kombe  hilo  miaka  minne  baadaye. Rais   wa  FIFA, Joseph Blatter,  anataka kuzipa  nchi  hizo  zitakazochaguliwa  nafasi  ya  muda  mrefu  wa kujitayarisha  na  ana matumaini  kuwa  hatua  hiyo  itasaidia   kupata wadhamini  wengi  kupitia  matangazo  na   televisheni .

Nchi  zinazowania   kuwa  wenyeji  wa  mashindano  hayo  kwa  ajili  ya fainali  za  mwaka  2018  ni  Uingereza, Urusi, Hispania  na  Ureno  na Ubelgiji  na  Uholanzi. Kwa  ajili  ya  fainali  za  mwaka  2022  wanaowania ni  pamoja  na  Marekani, Australia, Katar, Korea  ya  kusini  na  Japan. Muda wa  kuomba  kuwa  wenyeji   kumekuwa  na  mivutano  miongoni  mwa wagombea. Uchaguzi  huo  ambao  kura  ni  siri  nao  pia  umegubikwa  na shutuma   kadha   za  rushwa  dhidi  ya  wajumbe  wa kamati  hiyo  tendaji, Amos Amadu  kutoka  Nigeria  na  Reynald  Tenamrii  kutoka  Tahiti. Wajumbe  hao  wawili  wamesimamishwa  uwanachama  kutokana  na tuhuma  hizo. Kamati  hiyo  tendaji , ya  kile  kinachojulikana  kama   serikali ya  dunia  inayoongoza   soka,  ina  wajumbe  12,  ambapo ni  Franz Beckenbauer  atakuwa  mwanachama  wake  hadi  2011.

Katika  uchaguzi  huo  ni  wajumbe  22  tu  ambao  wanashiriki.  Hali  tayari ni  wazi  kuwa  fainali  za  kombe  la  dunia  kwa  mwaka  2018  zitafanyika baada  ya  miaka  12  katika  bara  la  Ulaya  tangu  yalipofanyika   nchini Ujerumani. Marekani   iliondoa   ombi  lake   la  kuwania  kuwa  mwenyeji wa  kinyang'anyiro  mapema  mwezi  wa  Oktoba. Zikabakia  nchi  kutoka katika  bara  la  Ulaya  pekee. Nchi  zinazoonekana  kuwa  mbele  kuweza kupata  kuwa  mwenyeji  wa  mashindano  hayo  ni  pamoja  na  Uingereza  na Urusi. Uingereza  iliwahi  kuwa  mwenyeji  wa  fainali  hizo  katika  mwaka 1966, na  mwaka  1996  iliwahi  kuwa  mwenyeji  wa  mashindano  ya fainali  za  kombe  la  mataifa  ya  Ulaya. Urusi  haijawahi  kuwa  mwenyeji wa  mashindano  yoyote  makubwa , na  inatarajiwa  kuwa   mwenyeji  wa mashindano  ya  Olympiki  ya  majira  ya  baridi  mwaka  2014. Katika mwaka  2012  nchini Uingereza  kutakuwa  na   mashindano  ya  majira  ya joto  ya   michezo  ya  Olympiki.

Uingereza  inataraji  kama  inavyojulikana  kuwa  ni  mama  wa  kandanda, kuwa  mwenyeji  wa  mashindano  hayo  kwa  mara  ya  pili, baada  ya ushindi  wake  wa   fainali  hizo  mwaka  1966.  Katika  fainali  iliishinda Ujerumani  kwa  mabao 4-2  baada  ya  dakika  za  nyongeza. Haitasahaulika lile  goli  linalojulikana  nchini  Ujerumani  kama  goli  la  Wembley, goli ambalo  lilibishaniwa, lililofungwa  na  Geoff Hurst . Timu  ya  taifa  ya Uingereza   tangu  wakati  huo  haijawahi  kulinyakua  tena  kombe  hilo, lakini  ushiriki  wa   nchi  hiyo  katika  mashindano  haya   haujasitishwa.

Urusi  inajiona  kuwa  ni  nchi  ambayo  inaweza  kuwa  mshindani  mkubwa wa  Uingereza  katika  kinyang'anyiro   hicho  cha  kuwania  kuwa  mwenyeji wa  mashindano  hayo. Tunataka  kuonyesha  hali  mpya  ya  Urusi , anasema waziri  wa  michezo  wa  Urusi , Vitali Mutko. Pia  tunataka  kujaribu kujenga  daraja  baina  ya  kile  watu  wanachokifahamu  kuhusu  Urusi   na hali  halisi  iliyopo. Hii  ni  nchi  ambayo  ina  sura  nyingi. Mfano  wetu tunaupata  kutoka  Ujerumani, amesisitiza  Mutko, kwamba  jinsi  Ujerumani ilivyochukulia  kwa  urahisi  kupata  ushindi  wao  ndivyo  ilivyokuwa  pia katika  kuendesha  mashindano  hayo  ya  fainali  za  mwaka  2006. Pamoja na  Urusi   na  Uingereza  kuna  nchi  kama  Ubelgiji  na  Uholanzi  ambazo zina  uzoefu  wa  kuwa  wenyeji  wa  mashindano  kama  hayo.

Mwandishi : Boettcher, Arnulf / Sekione  Kitojo/

Mhariri: Othman  Miraji.