1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BANJUL : Rais wa Gambia kushughulikia wala rushwa

24 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFU8

Rais Yahya Jammeh wa Gambia amesema hapo jana atamshughulikia ipasavyo kila mwenye kupatikana na hatia ya kula rushwa baada ya repoti aliyoiundia tume kuwashutumu maafisa kadhaa waandamizi wa serikali kwa ulaji rushwa.

Jammeh amesema katika taarifa atamshughulikia yoyote yule ambaye jina lake litajitokeza vibaya kwenye repoti hiyo na kwamba hakutakuwepo na gombe la kutolewa muhanga na hata kama mama yake atakuwemo kwenye kurasa hizo atamshughulikia.

Maafisa 27 wa serikali walioachiliwa huru kati ya 30 waliokamatwa kwa madai ya rushwa hapo Jumanne wamepewa siku 14 kulipa malimbizo yao ya kodi au kujieleza vipi wameweza kumudu kumiliki nyumba kadhaa au magari kwa kutegemea mishahara yao ya serikali.

Tume hiyo ilioundwa mwezi wa Julai mwaka jana kuchunguza rushwa miongoni mwa maafisa waandamizi wa serikali ikiwa ni pamoja na mawaziri wa zamani na wale wa hivi sasa imepewa jina la Operesheni Hakuna Muafaka na rais huyo wa Gambia.