BANJUL: Jammeh amebakia rais wa Gambia
24 Septemba 2006Nchini Gambia,rais wa sasa Yahya Jammeh ameshinda uchaguzi wa rais uliofanywa siku ya Ijumaa.Kwa mujibu wa halmashauri ya uchaguuzi,Jammeh amejikingia asili mia 67 ya kura zilizopigwa. Mpinzani wake mkuu,mwanasheria anaegombea haki za binadamu,Ousainou Darboe amepata asili mia 27.Kwa mujibu wa maafisa wa uchaguzi,ni watu wachache waliokwenda kupiga kura.Inasemekana kuwa asilimia 59 tu ya watu walioandikishwa,ndio walijitokeza kupiga kura zao.Tume ya wasimamizi iliyotumwa na Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi-ECOWAS yenye wanachama 15,imesema “uchaguzi huo ulifanywa katika hali ya uwazi na kwa njia ya kuaminika”.Jammeh alijinyakulia madaraka katika mapinduzi ya mwaka 1994 na aliweza kubakia na wadhifa wake katika chaguzi mbili zilizofuata katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.