BANGKOK:Waikubali ripoti ya umoja wa mataifa juu ya hali ya hewa
4 Mei 2007Matangazo
Zaidi ya wanasayansi 100 na wataalam wengine katika masuala ya mabadiliko ya hali nya hewa, wameidhinisha rasmi ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa katika kupambana na ongezeko la ujoto duniani.
Hatua hii imekuja baada ya siku tano za majadiliano ya kina kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa mjini Bangkok Thailand.
Ripoti ya Umoja w Mataifa inasema kuwa vita dhidi ya ongezeko la ujoto duniani inawezekana na kwamba teknolojia ya kazi hiyo inapatikana.
Mapendekezo hayo yalitayarishwa na kundi la wataalam waliyoteuliwa na Umoja wa mataifa.