SiasaBangladesh
Banghladesh yamuachia huru kiongozi wa chama cha kiislamu
12 Machi 2024Matangazo
Serikali ya Bangladesh imemuachilia huru kiongozi wa chama kikubwa cha kiislamu, miezi 15 tangu maafisa wa kupambana na ugaidi walipomkamata wakati alipoapa kushiriki maandamano ya kuipinga serikali.
Kuachiwa huru kwa mkuu wa chama cha Jamaat-e-Islami, Shafiqur Rahman, kunakuja wakati msuguano wa kisiasa ukipungua kufuatia ushindi wa nne mfululizo wa waziri mkuu Sheikh Hasina mnamo mwezi Januari mwaka huu.
Msemaji wa chama Matiur Akanda ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Rahman, mwenye umri wa miaka 65, aliachiliwa huru kutoka gereza lenye ulinzi mkali nje ya mji mkuu Dhaka jana Jumatatu, saa chache kabla ya mfungo wa mwezi wa Ramadhani kuanza katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya waislamu.