1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bandari za EU zaungana dhidi ya ulanguzi wa dawa za kulevya

25 Januari 2024

Umoja wa Ulaya, umezindua "Muungano wa Bandari za Ulaya" ili kuoanisha mbinu za kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya na kupambana na vituo vya upenyezaji wa dawa hizo kutoka kwa makundi ya wahalifu

https://p.dw.com/p/4be5m
Tani 4.5 za dawa za kulevya aina ya Cocaine kutoka Uruguay zanaswa mjini Hamburg nchini Ujerumani mnamo Julai 2019
Dawa za kulevya aina ya CocainePicha: German Custom/AP Photo/picture alliance

Uzinduzi wa muungano huo uliofanyika katika bandari ya Antwerp nchini Ubelgiji, lango kuu la uingizaji wa dawa za kulevya aina ya Cocaine barani Ulaya, ulihudhuriwa na mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya na wawakilishi kutoka bandari 16 za umoja huo, pamoja na mashirika ya usafiri wa baharini.

Muungano unahitajika kukabiliana na wahalifu

Kamishna wa mambo ya ndani katika Umoja wa Ulaya Ylva Johansson, amesema kwamba wanahitaji kuwa na muungano huo ili kukabiliana na mtandao huo wa wahalifu.

Bandari kuu za Ulaya zimekumbwa na ghasia kutoka kwa makundi ya mafia wa maeneo hayo walioazimia kudumisha biashara hiyo haramu yenye faida kubwa kwa njia yoyote ile.