1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ban kuhusu mzozo wa Sahara ya Magharibi

9 Aprili 2013

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito wa kuwepo juhudi za kimataifa kumaliza mgogoro wa Sahara ya Magharibi kutokana na hofu kuwa vita vya Mali vinaweza kusambaa hadi eneo hilo linalokaliwa na Morocco

https://p.dw.com/p/18CEL
A handout photograph made available by the Maghreb Arab Press Agency (MAP) on 08 November 2010 shows Moroccan security forces dismantling a tent camp on the outskirts of Laayoun, western Sahara's capital, on 08 November 2010. According to media reports, clashes have erupted between Moroccan security forces and protesters in Western Sahara on 08 November in which several people were killed, after Moroccan security forces dismantled tents of the 'Gdaim Izik' camp that was the site of an anti government protest. EPA/HANDOUT EDITORIAL USE ONLY
Lager in der Westsahara geräumtPicha: picture alliance/dpa

Ban ametoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuliongezea nguvu jeshi la kulinda amani linalohudumu Sahara ya Magharibi, ambako Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi Polisario, zimekuwa zikilumbana kwa zaidi ya miongo mwili na nusu kuhusiana na udhibiti wa eneo hilo.

Ban amesema katika ripoti iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama kuwa eneo la Sahel linahitaji suluhisho la haraka kuhusiana na mgogoro wa muda mrefu. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa Christopher Ross amekuwa akiandaa mazungumzo mapya katika kanda hiyo baina ya Morocco na Chama cha Polisario.

Mojawapo ya kambi za wakimbizi katika Sahara ya Magharibi
Mojawapo ya kambi za wakimbizi katika Sahara ya MagharibiPicha: DW

Wakati mgogoro unaoendelea nchini Mali, ambako wanajeshi wanaoongozwa na Ufaransa wanapambana na wanamgambo wa kiislamu wenye itikadi kali, ukigonga vichwa vya habari, viongozi wengi wa Afrika wanalichukulia eneo la Sahara ya Magharibi kuwa mgogoro uliosahaulika katika bara la Afrika. Morocco ilianza kulidhibiti eneo la Sahara ya Magharibi katika mwaka wa 1975 baada ya wakoloni wa Uhispania kuondoka.

Chama cha Polisario kilianza kulalamika kikitaka taifa huru hadi pale Umoja wa Mataifa uliposimamia mpango wa kusitisha mapigano katika mwaka wa 1991. Juhudi za kutafuta suluhisho kupitia mazungumzo ziligonga mwamba. Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi Polisario kilitaka jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa, MINUSRO, kuandaa kura ya maoni ili kuamua kuhusu mustakabali wa himaya hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta. Morocco inakubali tu kuwepo mamlaka mapana.

Morocco mwaka jana ilikataa kwa muda kushiriki katika mazungumzo la Ross, lakini mjumbe huyo amekuwa katika ziara yake ya kwanza rasmi katika Sahara ya Magharibi ambako ameripoti kuhusu ukosefu wa dalili za kuwepo suluhisho kuhusu mustakabali wa eneo hilo.

Wanajeshi wa kulinda amani MINUROSO katika Sahara ya Magharibi
Wanajeshi wa kulinda amani MINUROSO katika Sahara ya MagharibiPicha: AFP/Getty Images

Na wakati hayo yakijiri, takribani wanajeshi 1,000 wa Ufaransa wamefanya msako mkubwa katika bonde moja linaloaminika kuwa kambi ya wanamgambo wenye mafungamano la al-Qaeda karibu na mji wa Mali wa Gao. Operesheni hiyo inayoongozwa na jeshi la Ufaransa kwa jina Gustav, inahusisha vifaru, helikopta na ndege. Kamanda wa jeshi la nchi kavu nchini Mali Jenerali Benard Barrera amesema wamelizunguka bonde hilo kaskazini ya Gao.

Mji wa Gao ulikuwa ngome ya Kundi la waasi la MUJAO, mojawapo ya makundi ya wapiganaji wa kiislamu wenye itikadi kali ambayo yalitwaa upande wa kaskazini ya Mali hadi pale wanajeshi wanaoongozwa na Ufaransa walipowafurusha mjini humo mwezi Januari mwaka huu.

Wanajeshi wa Ufaransa watawasaka waasi katika bonde hilo kwa siku kadhaa zijazo kwa usaidizi wa wanajeshi wa Mali na polisi kwa kuingia katika kambi za wafugaji wa kuhamahama. Wakati huo huo, Ufaransa imeliondoa kundi lake la kwanza la wanajeshi kutoka nchini Mali. Mkuu wa jeshi amesema wanajeshi 100 wameelekea Cyprus ambako watakaa kabla ya kwenda Ufaransa.

Mwandishi. Bruce Amani/AFP

Mhariri: Iddi Sessanga