1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAMAKO-Waislamu 11 watupwa jela kwa kuwazuia watoto wao wasipatiwe chanjo ya polio.

11 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFER

Waislamu 11 ambao wanaosadikiwa ni wa kikundi cha itikadi kali,wamehukumiwa kifungo cha kati ya miezi sita na miaka mitatu jela na mahakama nchini Mali,baada ya kupatikana na hatia ya kuwazuia watoto wao wasipatiwe chanjo ya ugonjwa wa kupooza ama polio.

Waliohukumiwa ni pamoja na raia 9 wa Mali na wawili kutoka nchi jirani ya Burkina Faso.

Mshtakiwa mwengine raia wa Mali,aliachiliwa huru baada ya mahakama hiyo kumuona hakuwa akipinga chanjo hiyo kutolewa kwa watoto.

Jaji aliyeendesha kesi hiyo Sidiki Sanongo,amesema kuwa watu hao walitiwa hatiani kwa kukaidi sheria za nchi,kutokuwa watiifu na vitendo vyao amevifananisha na uasi baada ya kukataa watoto wao kupatiwa chanjo ya ugonjwa wa kupooza,kwa madai kuwa ni Mungu mwenyewe ndie anayewafanya watu waugue na ni huyohuyo atakayewaponyesha.