1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Ugaidi

Balozi za Marekani Dar es salaam, Nairobi ziliposhambuliwa

Sylvia Mwehozi
7 Agosti 2019

Imetimia miaka 21 tangu kutokea mashambulio ya bomu kwenye balozi za Marekani katika miji ya Nairobi na Dar es Salaam nchini Tanzania.

https://p.dw.com/p/3NUxE
Bildergalerie Kenia 50 Jahre Unabhängigkeit
Picha: AFP/Getty Images

Imetimia miaka 21 tangu kutokea mashambulio ya bomu kwenye balozi za Marekani katika miji ya Nairobi na Dar es Salaam nchini Tanzania. Kiasi ya watu 250 waliuawa kwenye mashambulio hayo mwaka 1998. Kwa sasa vikosi vya Marekani vimekuwa vikiendelea na mashambulizi ya angani nchini Somalia ambako wanajeshi wa umoja wa Afrika, AMISOM, wanapambana na wapiganaji wa Al Shabaab. Wakati huo imearifiwa kuwa huenda wahanga wa shambulio la mwaka 1998 la balozi za Marekani wakalipwa fidia na serikali ya Sudan kutokana na kwamba Osama bin Laden na washirika wake walijificha huko wakati wa maandalizi. Mahakama ya juu ya Marekani inasubiriwa kutangaza uamuzi wake mwezi Oktoba mwaka ujao. Hilo huenda likaiondoa Sudan kwenye orodha ya mataifa yanayowapa nafasi magaidi. Osama bin Laden aliuawa mwezi wa mei 2011.