1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baku. Waazerbaijan wapiga kura leo.

6 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELB

Wapiga kura katika jimbo la zamani la Urusi la Azerbaijan wanapiga kura leo kulichagua bunge lao jipya. Kura hiyo inaonekana kuwa mtihani mkubwa kwa serikali kuimarisha demokrasia. Kiasi cha wachunguzi wa kimataifa 1,000 wako nchini Azerbaijan wakiangalia uchaguzi huo.

Tayari wamekwisha eleza wasiwasi wao kuhusu uhalali wa uchaguzi huo , huku kukiwa na ripoti za maafisa wa serikali kuwabughudhi na kuwakamata baadhi ya wanachama wa vyama vya upinzani.

Kura ya maoni ya hivi karibuni inatabiri kuwa kutakuwa na ushindi wa wazi kwa chama tawala cha rais Ilham Aliyev.