Baku. Chama tawala kinaongoza katika uchaguzi.
7 Novemba 2005Kutokana na matokeo ya mwanzo ya uchaguzi, tume ya uchaguzi nchini Azerbaijan imekitangaza chama tawala kuwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa bunge uliofanyika jana Jumapili.
Hata hivyo wanasiasa wa vyama vya upinzani wameishutumu serikali kwa kile walichodai kuwa ni udanganyifu uliokithiri na wanatishia kupinga matokeo hayo.
Rais Ilham Aliyev , ambaye amerithi nafasi ya uongozi kutoka kwa baba yake 2003, amekana madai hayo na kuuita uchaguzi huo kuwa ni hatua kubwa mbele kwa nchi yake.
Mataifa ya magharibi yanataka uimara katika nchi hiyo ya Asia ya kati kwasababu bomba kubwa la kusafirishia mafuta linatarajiwa kuanza kusafirisha mafuta kwa ajili ya soko la dunia mwaka ujao.
Ujumbe wa shirika la OSCE linaloangalia uchaguzi huo utawasilisha mawazo yake kuhusu uchaguzi huo leo Jumatatu, wakati matokeo rasmi yatakapotangazwa.