1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baidoa. Somalia. Waislamu wataka kupambana na majeshi ya Ethiopia.

16 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCj0

Kiongozi wa ngazi ya juu wa Kiislamu nchini Somalia amesema jana kuwa wapiganaji wake hawana mpango wa kuishambulia serikali ya mpito ya nchi hiyo ya pembe ya Afrika lakini wanataka kuwashambulia wanajeshi wavamizi wa Ethiopia.

Sheikh Hassan Dahir Aweys amebeza kuwa ni domo kaya shutuma za Marekani kuwa kundi la kigaidi la al Qaeda limechukua udhibiti wa kundi hilo. Mashahidi na wataalamu wanasema kuwa maelfu ya wanajeshi wa Ethiopia wako nje na ndani ya mji wa Baidoa , ikiwa ni pamoja na kuwa na kikosi maalum cha ulinzi kwa rais wa Somalia Abdullahi Yussuf.