BAIDOA: Majeshi ya Ethiopia yameingia Somalia
9 Oktoba 2006Matangazo
Majeshi ya Ethiopia yanasemekana yamewasili katika mji wa Bur Hakaba nchini Somalia yakiungana na wanajeshi wa serikali ya mpito. Taarifa hiyo imethibitishwa na wakaazi wa mji huo pamoja na wanamgambo wa kiislamu wanaoudhibiti mji mkuu Mogadishu, mji wa Kismayu na maeneo mengine ya kusini.
Kuingia kwa wanajeshi wa Ethiopia katika mji wa Bur Hakaba, ulio kilomita 60 mashariki mwa mji wa Baidoa, ni kuisaida serikali ya mpito ya Somalia, inayoongozwa na rais Abdulahi Yusuf Ahmed, kutambuliwa kimataifa, na kukabiliana na wapiganaji wa kiislamu wenye siasa kali.