1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroBahamas

Bahamas yataka mjadala wa fidia ya utumwa

25 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Bahamas amesema ni wakati sasa wa Jumuiya ya Madola kutafuta "haki" kutokana na historia ya kikatili ya utumwa.

https://p.dw.com/p/4mCwz
Kwenye Mkutano wa Jumuiya ya Madola kunahimizwa mjadala wa fidia ya utumwa
Mataifa mengi yaliyoathiriwa na biashara ya utumwa yanayataka mataifa yaliyohusika kulipa fidia dhidi ya biashara hiyo haramuPicha: Dave Thompson/AP Photo/picture alliance

Amesema hayo wakati makoloni ya zamani ya Uingereza yakitaka kujadili suala la fidia na Mwanamfalme Charles katika mkutano muhimu hii leo.

Waziri Mkuu huyo Philip Davis amesema wakati umefika wa kuwa na mazungumzo ya kweli kuhusu namna wanavyoyashughulikia makosa haya ya kihistoria.

Alisema hayo alipozungumza na shirika la habari la AFP katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola nchini Samoa.

Mataifa mengi ya Kiafrika, Karibiki na Pasifiki yanapendelea kuona Uingereza na mataifa mengine yenye nguvu ya Ulaya yanalipa fidia ya kifedha ama kufanya marekebisho ya kisiasa kutokana na historia hiyo.