1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Wasunni wafurahia UN kuendelea kuwepo nchini Iraq

11 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaE

Wanasiasa wa Kisunni nchini Iraq wamelipokea kwa furaha azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutanua harakati za Umoja huo nchini Iraq, na kusaidia juhudi za kupunguza umwagaji mkubwa wa damu unaoendelea nchini humo.

Msemaji wa kundi la wabunge wa Kisunni Salim Abdullah amesema kuwa Umoja wa mataifa ni chombo kisichoegemea upande wowote ambacho kinaweza kutoa mchango mkubwa nchini Iraq.

Baraza la Usalama la Umoja huo wa Mataifa hapo jana lilipitisha azimio la kuendelea kwa mwaka mmoja zaidi harakati za umoja huo nchini Iraq ambazo muda wake ulimalizika jana.