1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Gavana na Mkuu wa Polisi wauawa katika shambulizi la bomu nchini Iraq

11 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBa9

Gavana na Mkuu wa Polisi wa jimbo la Diwaniyah la kusini mwa Iraq wameuawa katika shambulizi la bomu la kutegwa bembezoni mwa barabara saa chache zilizopita.

Mkuu wa jeshi katika jimbo hilo, Brigadier Generali Othman al Farood amesema kuwa Gavana huyo Khalil Jalil Hamza na Mkuu wa Polisi Meja Generali Khalid Hassan waliuawa wakati msafara wao uliposhambuliwa kwa bomu kubwa lililotegwa pembeni ya barabara.

Katika shambulizi hilo lililotokea kwenye mjini mkuu wa jimbo hilo Ajjaf kiasi cha kilomita 130 kusini mwa Baghdad dereva na walinzi wa maafisa hao pia waliuawa.

Jimbo hilo la Diwaniyah linalokaliwa na idadi kubwa ya washia, limekuwa katika mapigano makali kati ya majeshi ya Marekani na wanamgambo wa kishia.