Baghdad. Wajumbe wa Kikurd wataka Uislamu usiwe chanzo kikuu cha sheria.
20 Agosti 2005Wajumbe wa Kikurd waliomo katika majadiliano juu ya katiba mpya nchini Iraq wamesema leo kuwa wataachana na madai yao ya kujitenga , lakini wanapinga vikali kuwa Uislamu uwe chanzo kikuu cha sheria hata kama Marekani imepunguza upinzani wake juu ya kuingiza dini katika katiba hiyo mpya.
Mahmud Othman , mjumbe wa Kikurd katika kamati hiyo ya kutunga katiba ameliambia shirika la habari la AFP kuwa iwapo tutaona kuwa haki ya kuwa na taifa letu inakuwa kipingamizi katika kukamilisha utungaji wa katiba hiyo , bunge letu litakuwa litalegeza msimamo na kujiondoa katika hali ya kuwa kikwazo.
Duru za karibu na majadiliano hayo ya kutunga katiba zimesema kuwa majadiliano hayo yalianza upya baada ya Marekani kuacha upianzani wake kuingiza Uislamu kuwa sehemu muhimu ya sheria za Iraq.