1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Ulinzi kuimarishwa Iraq ikicheza fainali

29 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeG

Vikosi vya ulinzi vya Iraq vimesema hapo jana vina mipango ya kuwalinda mashabiki wa soka walioazimia kusheherekea kuingia kwenye fainali kwa timu ya Iraq katika historia ya michuano ya ubingwa wa Kombe la Asia licha ya kufanyika kwa mashambulizi mabaya ya kujitolea muhanga maisha kufuatia mchezo wao wa mwisho.

Msemaji mkuu wa jeshi la Iraq Generali Qassim Atta amesema wahusika wote wanajiandaa kukabiliana na uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi dhidi ya watu wanaoshehereka mpambano wa leo wa fainali kati ya Saudi Arabia na Iraq unaofanyika mjini Jakarta Indonesia.

Iraq imeingia nusu fainali hiyo baada ya kuitowa Korea Kusini kwa penelti hapo Jumaatano ushindi ambao ulipelekea maelfu kumiminika Baghdad kusheherekea na kuja kuripuliwa kwa mashambulizi ya kujitokea muhanga maisha yaliogharimu maisha ya watu 50.