Baghdad. Picha za Saddam akiwa na chupi tu kuchapishwa tena na gazeti la Sun leo Jumamosi.
21 Mei 2005Mawakili wanaomtetea rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein wanasema kuwa wanafikiria kuchukua hatua za kisheria dhidi ya gazeti moja la Uingereza ambalo limechapisha picha za kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani akiwa ameva chupi tu katika chumba alimofungiwa.
Gazeti la Sun ambalo linahusika na uchapishaji wa picha hizo, limesema kuwa litapambana na hatua yoyote ya kisheria dhidi yake, na kuongeza kuwa linapanga kuchapisha picha nyingine zaidi leo Jumamosi.
Maafisa wa Marekani wamesema kuwa uchapishaji wa picha hizo unaweza kuwa unakwenda kinyume na sheria za mkataba wa Geneva kuhusiana na utendewaji kinyume na ubinadamu wafungwa wa kivita.
Saddam Hussein anashikiliwa na majeshi ya Marekani katika eneo ambalo halifahamiki nchini Iraq wakati akingojea kesi yake dhidi ya madai kadha.