1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD :Mwandishi habari wa Italia aachiliwa huru

5 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZZ

Mwandishi wa habari wa Kitaliana Giuliana Sgrena ameachiliwa huru na watekaji wake hapo jana lakini wanajeshi wa Marekani wameufyetulia risasi kwa makosa msafara wake ambapo wamemjeruhi mwandishi huyo wa kike pamoja na kumuuwa jasusi wa Italia.

Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi mmojawapo wa waungaji mkono wakuu wa Rais George W Bush nchini Iraq kwa haraka amemwita balozi wa Marekani na kutaka ufafanuzi pamoja na kuwajibishwa kwa wahusika wa tukio hilo.

Wanajeshi wa Marekani walimuuwa jasusi huyo kwenye kituo cha ukaguzi wa kijeshi na kumjeruhi Sgrena begani wakati akipelekwa uwanja wa ndege wa Baghdad baada ya kuachiliwa na kukabidhiwa kwa maafisa wa ujasusi watatu wa Italia.

Sgrena mwenye umri wa miaka 57 anayefanya kazi na gazeti la Kikomunisti la Manifesto lenye makao yake mjini Rome alitekwa nyara hapo Februari 4 wakati akifanya mahojiano mitaani karibu na Chuo Kikuu cha Baghdad.