1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD Mateka wa rehani wa Italia ataka wanajeshi wa Italia waondoke Irak.

17 Februari 2005
https://p.dw.com/p/CFd6

Mwandishi habari wa Itali, Giuliani Sgrena, aliyetekwa nyara mjini Baghdad, nchini Irak, mapema mwezi huu, ameonyeshwa kwenye ukanda wa video akita aokolewe, na wanajeshi wa Itali walio nchini humo waondoke mara moja. Ukanda huo ambao haijulikani ni lini ulipotayarishwa ulitolewa jana na kundi la wapiganaji wanaomzuilia mwandishi huyo. Serikali ya Itali imetangaza kuwa haitolipa fedha zozote kwa wapiganaji hao ili Giuliani aachiliwe huru. Tangazo hili limefanywa baada ya bunge la nchi hiyo kupiga kura kurefusha muda wa tume ya wanajeshi wake walio nchini Irak, ambao ulitarajiwa kumalizika mwezi Juni.