1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Kiongozi wa al Qaeda awataka wanasayansi wasaidie

29 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD7i

Kiongozi wa Al Qaeda nchini Irak amewatolea mwiti wanasayansi wachangie katika mashambulio nchini humo kwa kusaidia kuvumbua silaha za maangamizo ya halaiki.

Katika ukanda wake wa video uliotumwa kwenye mtandao wa internet, Abu Hamza al Muhajer pia amewataka wapigajai wawateke nyara wakristo wa mataifa ya magharibi walio Irak.

Miito hiyo imetolewa huku wimbi la machafuko ya kikablia likizidi wakati wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani na raia George W Bush wa Marekani akikosolewa kwa anavyovishuhgulikia vita vya Irak.

Hii leo maiti nane zilizokuwa na lama za mateso zimepatika mjini Baghdad.

Wakati huo huo shemegi wa Saddam Hussein ameuwawa leo kwa kupigwa risasi mjini Baghdad. Binamu wa jaji anayeongoza kesi ya Saddam amejeruhiwa katika isa hicho.

Haikubanika wazi ikiwa shambulio hilo linahusiana na jaji Mohamed Oreibi afl Khalifa, aliyechukua uongozi katika kesi ya Saddam juma lililopita.