1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Kesi ya mauaji ya Wakurdi yasikilizwa leo

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcR

Kesi ya mauaji ya wakurdi inayowakabili maofisa sita wa serikali ya zamani ya Irak inatarajiwa kuanza tena leo mjini Baghdad bila kiongozi wa zamani wa Irak Saddam Hussein.

Mtuhumiwa mkuu katika kesi hiyo ni Ali Hassan al Majid anayejulikana kwa jina maarufu la Chemical Ali. Al Majid anashtakiwa kwa kuwaua wakurdi 180,000 katika miaka ya 1980.

Watuhumiwa wengine watano wanashtakiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. Iwapo watapatikana na hatia, watuhumiwa wote sita huenda wahukumiwe kunyongwa.