1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Jeshi la Marekani lakana taarifa ya Al Qaeda.

3 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEVR

Taarifa ya kundi la kigaidi la mtandao wa al Qaeda kuwa wanajeshi wawili wa Marekani wanashikiliwa na kundi hilo imekanushwa na msemaji wa jeshi la Marekani.

Al Qaeda limedai katika taarifa ya internet kuwa wanajeshi wawili wa Marekani watauwawa iwapo wafungwa wa Kissuni wanawake hawataachiwa kutoka jela katika muda wa saa 24.

Majeshi ya Marekani yamefanya mashambulio makubwa katika eneo la magharibi ya Iraq karibu na mpaka na Syria wiki hii yakiwalenga wapiganaji wa kundi la al Qaeda.

Wakati huo huo maafisa wa Kishia wametangaza kuwa kaka wa waziri wa mambo ya ndani wa Iraq ambaye alitekwa nyara na watu wenye silaha siku ya Jumamosi, ameachiliwa huru.