Baa la njaa na ukame lasababisha wimbi la wakimbizi nchini Kenya
11 Julai 2011Matangazo
Hali mbaya ya ukame iliyozikumba nchi za eneo la Pembe ya Afrika Ethiopia Djibouti na Somalia, pamoja pia na eneo la Kaskazini mwa Kenya imesababisha maelfu ya watu kuzikimbia nyumba zao kila siku na kwenda kutafuta hifadhi katika makambi ya wakimbizi, ambako wanaweza kupata msaada wa chakula.
Kambi ya wakimbizi ya Dadaab nchini Kenya kwa sasa imekuwa ikipokea wakimbizi hao wanaokimbia makaazi yao kutokana na Ukame na njaa hasa kutoka nchini Somalia.