MigogoroYemen
Azimio la UN la laani hujuma za waasi wa Houthi
11 Januari 2024Matangazo
Azimio hilo lililoandaliwa kwa pamoja na Marekani na Japan linasema hujuma zinazofanywa na waasi wa Houthi zinateteresha biashara ya ulimwengu na kutishia usalama na amani kwenye kanda ya Mashariki ya Kati.
Waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran na ambao wamekuwa wakipigana vita tangu mwaka 2014 dhidi ya serikali inayotambuliwa kimataifa nchini Yemen, wamesema wanafanya mashambulizihayo kwa lengo la kushinikiza kusitishwa kampeni ya kijeshi ya Israel huko Ukanda wa Gaza.
Msemaji wa kundi hilo la waasi Mohammed Ali al-Houthi amepuuza azimio lililopitishwa jana akilitaja kuwa "mchezo wa kisiasa" na kuituhumu Marekani kuwa ndiyo inakiuka sheria za kimataifa.