1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azimio la baraza la usalama kwa Myanmar

12 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7GR

New-York:

Urusi na China,mataifa mawili ,kati ya matano yanayomiliki kura ya turufu katika baraza la usalama la Umoja wa mataifa,yamezuwia azimio linalolaani vikali uamuzi wa serikali ya Myanmar wa kukandamiza maandamano ya amani nchini humo.Badala yake taasisi hiyo muhimu ya umoja wa mataifa imepitisha azimio dhaifu tuu linazungumzia juu ya “masikitiko kwa kutumiwa nguvu dhidi ya waandamanaji.”Wanachama kumi na watano wa baraza la usalama wametoa mwito wa kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa nchini Myanmar.Kinyume na mswaada wa awali wa azimio hilo,tafsiri hii ya mwisho haitilii mkazo kiongozi wa upinzani Aung San Suu Kyi aachiwe huru.Baraza la usalama la umoja wa mataifa limewatolea mwito watawala wa kijeshi”wazungumze na upande wa upinzani.