MigogoroAzerbaijan
Azerbaijan yakataa kushiriki mazungumzo ya amani na Armenia
16 Novemba 2023Matangazo
Azerbaijan imesema Marekani ina msimamo wa upendeleo. Wizara ya mambo ya kigeni ya Azerbaijan imesema haioni kama inawezakana kufanyika mkutano huo unaopendekezwa wa ngazi ya Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa jamhuri hizo mbili za uliokuwa muungano wa Sovieti mjini Washington Novemba 20.
Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan amesema leo kwamba "nia ya kisiasa ya Yerevan ya kutia saini, katika miezi ijayo, makubaliano ya amani na Azerbaijan bado haitetereki."
Azerbaijan na Armenia zimekuwa kwenye mgogoro wa mipaka uliodumu kwa miongo kadhaa kuhusiana na mkoa wa Azerbaijan wa Nagorno-Karabakh, ambao Baku iliukomboa Septemba mwaka huu baada ya operesheni kali ya kijeshi dhidi ya wanaharakati wa Kiarmenia wanaopigania kujitenga.