Azerbaijan kutoa pendekezo jipya la ufadhili wa tabianchi
22 Novemba 2024Mataifa yamegawanyika kuhusu makubaliano ya ufadhili wa dola trilioni moja, yanayotarajiwa kuchukua nafasi ya ahadi ya kila mwaka ya dola bilioni 100 iliyotolewa na mataifa tajiri kusaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Azerbaijan ambayo ndio inashikilia urais wa COP29 imesema katika taarifa kuwa "imetiwa moyo na kiwango cha wepesi kinachooneshwa na washiriki” na itatoa rasimu mpya leo Ijumaa.
Soma pia: Dunia bado imegawanyika kuhusu fedha wakati muda ukiyoyoma COP29
Azerbaijan ambayo ndio inashikilia urais wa COP29 imesema katika taarifa kuwa “imetiwa moyo na kiwango cha wepesi kinachooneshwa na washiriki” na itatoa rasimu mpya Ijumaa. Rasimu hiyo mpya inatarajiwa kutoa takwimu za kifedha baada ya waraka wa awali uliotolewa jana Alhamisi kusema kuwa nchi zinazoendelea zilihitaji angalau dola trilioni fulani kwa mwaka lakini ikaondoa kiasi kamili cha fedha.