Haki sawaAustralia
Australia kutangaza kura ya maoni kutambua jamii ya asili
30 Agosti 2023Matangazo
Raia wa Australia wataulizwa iwapo wanaunga mkono kubadilishwa kwa katiba na kujumuisha kile kilichoitwa "Sauti kwa Bunge," kamati ya watu wa jamii ya asili ili kulishauri bunge juu ya masuala yanayoathiri watu wa jamii ya Aboriginal na wale wa visiwa vya Torres Strait.
Mabadiliko yoyote ya kikatiba nchini Australia yanahitaji kura ya maoni ya kitaifa.
Nchi hiyo haina mkataba wa aina yoyote na watu wake wa asili ambao ni asilimia 3.2 tu ya idadi jumla ya watu milioni 26 nchini humo na aghalabu huishi katika umaskini mkubwa.
Jamii hizo za watu wa asili pia hawajatajwa kwenye katiba licha ya kuishi Australia kwa zaidi ya miaka 60,000.