1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AUSCHWITZ. Kumbukumbu za mauaji ya halaiki ya wayahudi.

5 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFGW

Maelfu ya wayahudi na raia wengine wasio wayahudi wanaandamana katika kambi ya mateso ya Auschwitz Birkenau hii leo kuwakumbuka mamilioni ya wayahudi waliouwawa katika mauji ya halaiki ya wayahudi.

Viongozi kutoka mataifa mbalimbali pia wanashiriki katika maandamano hayo ya kila mwaka ya kilomita tatu, ambayo yanatarajiwa kuwa makubwa zaidi katika historia, miaka 60 tangu kukombolewa kwa kambi za mateso.

Waziri mkuu wa Israel, Ariel Sharon na waziri mkuu wa Poland, Marek Belka, watatoa hotuba zao kuitolea wito jamii ya kimataifa kutoisahau hofu ya mauaji hayo.