Augsburg, Ujerumani. Waziri wa zamani aenda jela kwa hongo.
13 Agosti 2005Matangazo
Mahakama moja katika mji wa kusini mwa Ujerumani wa Augsburg imemhukumu naibu waziri wa zamani wa ulinzi Holger Pfahls kwenda jela miaka miwili na miezi mitatu kwa makosa ya kupokea hongo na kukwepa kodi.
Bwana Pfahls mwenye umri wa miaka 62 amekiri kupokea kiasi cha Euro milioni mbili katika mpango wa kuuza magari ya kijeshi kwa Saudi Arabia mwaka 1991.
Pia amekiri kuwa alishindwa kutoa maelezo ya mapato yake hayo.
Pfahls alikamatwa mjini Paris katikati ya mwaka jana , baada ya kuwakwepa maafisa wa jeshi la polisi wa Ujerumani kwa muda wa miaka mitano.