AUGSBURG. mahakama tayari kutoa uamuzi
12 Agosti 2005Mahakama ya Augsburg kusini mwa Ujerumani inajitayarisha kutoa hukumu ya kesi ya rushwa inayomkabili naibu wa waziri wa zamani katika wizara ya ulinzi.
Viongozi wa mashtaka wanapendekeza bwana Holger Pfahls mwenye umri wa miaka 62 apewe adhabu ya kifungo cha miaka miwili na miezi mitatu gerezani.
Bwana Holger amekiri kupokea takriban Euro milioni mbili katika mpango wa vifaru 36 kwa Saudi Arabia na kisha kushindwa kutoa habari katika idara ya kodi juu ya fedha hizo.
Wiki mbili zilizopita katika ushahidi wake kansela wa zamani Helmut Kohl aliiambia mahakama kuwa Holger Pfahls hakuhusika na ushawishi wa aina yoyote katika mpango wa vifaru kwa Saudi Arabia.
Bwana Pfahls alikamatwa mjini Paris Ufaransa katika msimu wa kiangazi uliopita baada ya kuwakwepa polisi wa Ujerumani kwa kipindi cha miaka mitano.