AU yachelewesha matumizi ya fedha kwa operesheni za usalama
11 Februari 2020Matangazo
Umoja wa Afrika (AU) ambayo ina nchi 55 wanachama, ilitaraji kuanza kuzitumia fedha za mfuko huo mwaka huu kwa operesheni za kulinda amani, juhudi za maridhiano na kuzuia migogoro kwenye bara ambalo linakabiliwa na vitisho vya machafuko na ugaidi.
Lakini baada ya kukamilika mkutano wake mjini Addis Ababa Ethiopia, viongozi hao wameamua kutoanza kutumia hazina hiyo baada ya kuibuka kuwa ina chini ya nusu ya dola milioni 400 ilizolenga kupata.
Mataifa ya Afrika kaskazini, zikiwemo Misri na Algeria, yanapinga michango yao ya kila mwaka na yanataka mataifa ya Arika ya Kati kama vile Cameroon na Jamhuri ya Afrika ya Kati kutoa mchango mkubwa.