ATHENS: AC Milan yanyuka Liverpool mabao 2-1 na kutwaa ubingwa wa Ulaya
24 Mei 2007Matangazo
Klabu ya AC Milan jana usiku ilitawazwa kuwa mabingwa wa Ulaya baada ya kuikandika Liverpool mabao mawili kwa moja kwenye mechi ya fainali iliyochezewa mjini Athens, Ugiriki.
Mambo yote mawili ya Milan yalitiwa kimiani na Filippo Inzaghi.
Ushindi huo una maana kwamba AC Milan imelipiza kisasi cha mwaka 2005 mjini Istanbul, Uturuki, iliposhindwa na Liverpool kwa mikwaju ya penalti .