1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Atalanta ya Italia yacheza chini ya kiwingu cha corona

25 Juni 2020

Ligi ya Serie A ya Italia ni miongoni mwa ligi zilizoanza kuchezwa tena wakati wa janga la virusi vya corona. Hii inajumuisha Atalanta, ambayo mechi yake ya ligi ya mabingwa Ulaya inafikiriwa kuwa kubwa huko Bergamo.

https://p.dw.com/p/3eJAe
Italien Fussball Atalanta vs. Sassuolo
Picha: picture-alliance/AP Photo/L. Bruno

Kiwanja kilicho mbele ya uwanja wa michezo wa Gewiss mjini Bergamo hakina watu. Mashabiki wapatao 150 kutoka Curva kaskazini wamekusanyika mbele ya baa iliyopo karibu na uwanja huo, mahala ambapo kawaida huwa wanakutana kabla ya mechi. Wameshika mabango sio kwa ajili ya kuishangilia timu yao wanayoipenda ya Atalanta, bali kulaani kuanza tena kwa ligi ya Serie A wanakosema ni "aibu”.

"Ni aibu, ni aibu” mashabiki waliimba mbele ya lango kuu la kuingilia uwanjani huku wakiwa wameshika mabango miongoni mwa mabango hayo yakiwa yameandikwa mpira wa miguu bila ya kuwa na mashabiki hakuna mpira wa miguu.

Wakati huo huo gazeti la kila siku la dello sport linaadhimisha ushindi wa Atalanta baada ya kuifunga mabao 4-1 timu ya Sassuolo kana kwamba mechi hiyo ilikuwa tukio kuu. Lakini kuanza tena kwa mechi za soka huko Bergamo ni habari kubwa zaidi kuliko kilichotokea uwanjani. Siku 103 zimepita tangu Atalanta iibuke na ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Valencia katika mashindano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mechi inayoelezwa kuharakishwa kuenea kwa virusi vya corona na kugeuza Bergamo kuwa sehemu kubwa ya janga hili.

Nani angesahau picha za malori ya jeshi la Italia kusafirisha mamia ya majeneza nje ya mji kwa sababu nafasi ya kuzikia miili ya watu ilikosekana? Takribani watu 6,000 walifariki dunia mnamo mwezi Machi mwaka huu.

(ape)