ASTANA: Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amewasili Kazakhastan
4 Desemba 2003Matangazo
kwa ziara ya kwanza ikifanywa na mkuu wa serikali ya Ujerumani. Katika mji mkuu Astana wa Jamhuri hiyo ya Eshia ya Kati, alipokelewa rasmi na rais NURSULTAN NAZARBAYEV. Wakati wa kuzungumza na uongozi wa Kasakhstan, mada kuu ni kutanua uhusiano wa kibiashara baina ya nchi mbili. Bwana Schroeder anaandamana na waziri wa vyombo vya uchukuzi, Manfred Stolpe, na wawakilishi 11 wa makampuni ya kijerumani. Hapo awali akiwa na ziara ya China, Bwana Schroeder alitoa mwito kikwazo cha silaha cha Muungano wa Ulaya ilichoekewa China, kiondolewe kabisa.