ASMARA:Watu 400 warejeshwa kwao Ethiopia na Eritrea
29 Januari 2007Matangazo
Kamati ya Kitaifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu imewarejesha watu mia nne nchini Ethiopia na Eritrea zinazozonia eneo la mpakani kati yao.Watu zaidi ya mia tatu ya wote wakiwemo watoto walivuka mpaka kutoka Eritrea hadi Ethiopia katika eneo la Mto Mereb.
Kwa mujibu wa Shirika hilo shughuli hiyo ilifanyika kukiwa na ushirikiano na serikali zote mbili.Mataifa hayo jirani yamekuwa yakiwafurusha maelfu ya watu wanaodhania kuwa maadui wao tangu vita kati yao kuhusu eneo la mpakani la Badme mwaka 98 hadi 2000.Mzozo huo wa mpaka bado haujatatuliwa mpaka sasa.