1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASMARA:Achaguliwa kuongoza mapambano ya kuikomboa Somalia

25 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBMt

Muungano mpya wa kiislam nchini Somalia umemteua mbabe wa kivita mwenye nguvu kubwa, Sheikh Yusuf Mohamed Siad kuongoza mapambano dhidi ya majeshi ya Ethiopea nchini humo.

Sheikh Yusuf ambaye ni waziri wa zamani wa ulinzi katika muungano uliyofurushwa wa mahakama za kiislam, alichaguliwa kushika nafasi hiyo tena katika muungano huo mpya ulianzishwa kuikomboa Somalia.

Afisa wa juu wa muungano huo uliyoanzishwa uhamishoni nchini Eritrea, Zakariya Mahamud Abdi amesema kuwa Sheikh Yusuf kwa sasa yuko mjini Mogadishu akiongoza mapambano yaliyoanza Jumapili dhidi ya serikali ya mpito inayoungwa mkono na majeshi ya Ethiopea.

Wapiganaji wa muungano hao walianzisha mashambulizi baada ya kuishambulia kambi moja ya kijeshi ambapo watu sita waliuawa wakiwemo askari wanne wa serikali.