1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ASMARA: Wapinzani wa Somalia wakutana Eritrea

5 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBSb

Viongozi wa upinzani wa Somalia wanakusanyika katika mji mkuu wa Eritrea,Asmara kutayarisha mkutano wa siku ya Alkhamisi.Kwa mujibu wa viongozi wa Kisomali waliowasili Asmara,lengo la mkutano huo ni kuunda ushirikiano wa upinzani kuikomboa Somalia kutoka uvamizi wa Ethiopia na washirika wake.Hadi wajumbe 450 wanatazamiwa kuhudhuria mkutano huo wa siku 10 mjini Asmara.