ASMARA: Hatima ya raia 8 wa Ethiopia haijulikani
14 Machi 2007Matangazo
Wazungu 5 walioachiliwa huru baada ya kuzuiliwa kwa takriban majuma mawili nchini Ethiopia sasa wanapumzika katika ubalozi wa Uingereza nchini Eritrea wakitazamiwa kurejea nyumbani hivi karibuni.Waingereza wanne na mwanamke mmoja wa Kifaransa walichukuliwa mateka tarehe mosi mwezi Machi,walipokuwa wakitembelea eneo la ndani la Afar,kaskazini mwa Ethiopia.Hatima ya raia 8 wa Ethiopia waliyokamatwa wakati mmoja na wazungu hao,haijulikani.