1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Asmara. Ethiopia yashutumiwa kwa uhalifu wa kivita Mogadishu.

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC66

Eritrea imeishutumu nchi jirani ya Ethiopia kwa kufanya kampeni ya kuipaka matope jana Jumamosi , na kuonya kuwa Ethiopia inachochea hali ya wasi wasi kati ya mataifa hayo mawili ya pembe ya Afrika.

Ikipuuzia madai ya Ethiopia ya kwamba Eritrea inakumbatia magaidi ikiwa ni njia ya kujiondolea mzigo wa hali ya wasi wasi nchini mwake na mgogoro wa mapigano nchini Somalia. Wizara ya mambo ya kigeni ya Eritrea imeishutumu nchi hiyo jirani kwa uhalifu mkubwa wa kivita mjini Mogadishu.